Qad Khasira Al-Ladhīna Kadhdhabū Biliqā'i Allāhi Ĥattaá 'Idhā Jā'at/hum As-Sā`atu Baghtatan Qālū Yā Ĥasratanā `Alaá Mā Farraţnā Fīhā Wa Hum Yaĥmilūna 'Awzārahum `Alaá Žuhūrihim 'Alā Sā'a Mā Yazirūna (Al-'An`ām: 31). |
31. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba. |