Mā Al-Masīĥu Abnu Maryama 'Illā Rasūlun Qad Khalat Min Qablihi Ar-Rusulu Wa 'Ummuhu Şiddīqatun Kānā Ya'kulāni Aţ-Ţa`āma Anžur Kayfa Nubayyinu Lahum Al-'Āyāti Thumma Anžur 'Annaá Yu'ufakūna (Al-Mā'idah: 75). |
75. Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyo wabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa. |