Wa Qaffaynā `Alaá 'Āthārihim Bi`īsaá Abni Maryama Muşaddiqāan Limā Bayna Yadayhi Mina At-Tawrāati Wa 'Ātaynāhu Al-'Injīla Fīhi Hudan Wa Nūrun Wa Muşaddiqāan Limā Bayna Yadayhi Mina At-Tawrāati Wa Hudan Wa Maw`ižatan Lilmuttaqīna (Al-Mā'idah: 46). |
46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu. |