Wa Yastaftūnaka Fī An-Nisā' Qul Allāhu Yuftīkum Fīhinna Wa Mā Yutlaá `Alaykum Fī Al-Kitābi Fī Yatāmaá An-Nisā' Al-Lātī Lā Tu'utūnahunna Mā Kutiba Lahunna Wa Targhabūna 'An Tankiĥūhunna Wa Al-Mustađ`afīna Mina Al-Wildāni Wa 'An Taqūmū Lilyatāmaá Bil-Qisţi Wa Mā Taf`alū Min Khayrin Fa'inna Allāha Kāna Bihi `Alīmāan (An-Nisā': 127). |
127. Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua. |