Fa'idhā Qađaytum Aş-Şalāata Fādhkurū Allāha Qiyāmāan Wa Qu`ūdāan Wa `Alaá Junūbikum Fa'idhā Aţma'nantum Fa'aqīmū Aş-Şalāata 'Inna Aş-Şalāata Kānat `Alaá Al-Mu'uminīna Kitābāan Mawqūtāan (An-Nisā': 103). |
103. Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala. Na mtapo tulia basi shikeni Sala kama dasturi. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu. |