'Inna Al-Ladhīna Tawaffāhum Al-Malā'ikatu Žālimī 'Anfusihim Qālū Fīma Kuntum Qālū Kunnā Mustađ`afīna Fī Al-'Arđi Qālū 'Alam Takun 'Arđu Allāhi Wāsi`atan Fatuhājirū Fīhā Fa'ūlā'ika Ma'wāhum Jahannamu Wa Sā'at Maşīrāan (An-Nisā': 97). |
97. Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa. |