Faqātil Fī Sabīli Allāhi Lā Tukallafu 'Illā Nafsaka Wa Ĥarriđ Al-Mu'uminīna `Asaá Allāhu 'An Yakuffa Ba'sa Al-Ladhīna Kafarū Wa Allāhu 'Ashaddu Ba'sāan Wa 'Ashaddu Tankīlāan (An-Nisā': 84). |
84. Basi pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hukalifishwi ila nafsi yako tu. Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulio ya walio kufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu. |