Wa 'Idhā Jā'ahum 'Amrun Mina Al-'Amni 'Aw Al-Khawfi 'Adhā`ū Bihi Wa Law Raddūhu 'Ilaá Ar-Rasūli Wa 'Ilaá 'Ūlī Al-'Amri Minhum La`alimahu Al-Ladhīna Yastanbiţūnahu Minhum Wa Lawlā Fađlu Allāhi `Alaykum Wa Raĥmatuhu Lāttaba`tum Ash-Shayţāna 'Illā Qalīlāan (An-Nisā': 83). |
83. Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu. |