Mā Kāna Allāhu Liyadhara Al-Mu'uminīna `Alaá Mā 'Antum `Alayhi Ĥattaá Yamīza Al-Khabītha Mina Aţ-Ţayyibi Wa Mā Kāna Allāhu Liyuţli`akum `Alaá Al-Ghaybi Wa Lakinna Allāha Yajtabī Min Rusulihi Man Yashā'u Fa'āminū Billāhi Wa Rusulihi Wa 'In Tu'uminū Wa Tattaqū Falakum 'Ajrun `Ažīmun ('āli `Imrān: 179). |
| 179. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema. Wala haiwi kwa Mwenyezi Mungu kukujuulisheni mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume wake amtakaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume yake. Na mkiamini na mkamchamngu mtakuwa na ujira mkubwa. |