|
154. Kisha baada ya dhiki alikuteremshieni utulivu
- usingizi ambao ulifunika kundi moja kati yenu. Na kundi jengine nafsi
zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa
ya haki, dhana ya kijinga. Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo
hili? Sema: Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao
wasiyo kubainishia. Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili
tusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli
toka walio andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni
hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe
yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.
|