Sanulqī Fī Qulūbi Al-Ladhīna Kafarū Ar-Ru`ba Bimā 'Ashrakū Billāhi Mā Lam Yunazzil Bihi Sulţānāan Wa Ma'wāhum An-Nāru Wa Bi'sa Mathwaá Až-Žālimīna ('āli `Imrān: 151). |
| 151. Tutazitia khofu nyoyo za walio kufuru kwa vile walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote. Na makaazi yao ni Motoni; na maovu yaliyoje maskani ya wenye kudhulumu! |