Wa A`taşimū Biĥabli Allāhi Jamī`āan Wa Lā Tafarraqū Wa Adhkurū Ni`mata Allāhi `Alaykum 'Idh Kuntum 'A`dā'an Fa'allafa Bayna Qulūbikum Fa'aşbaĥtum Bini`matihi 'Ikhwānāan Wa Kuntum `Alaá Shafā Ĥufratin Mina An-Nāri Fa'anqadhakum Minhā Kadhālika Yubayyinu Allāhu Lakum 'Āyātihi La`allakum Tahtadūna ('āli `Imrān: 103). |
103. Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka. |