Ash-Shahru Al-Ĥarāmu Bish-Shahri Al-Ĥarāmi Wa Al-Ĥurumātu Qişāşun Faman A`tadaá `Alaykum Fā`tadū `Alayhi Bimithli Mā A`tadaá `Alaykum Wa Attaqū Allāha Wa A`lamū 'Anna Allāha Ma`a Al-Muttaqīna (Al-Baqarah: 194). |
194. Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu. |